Shushu Joel,Busega Busega.
Mgombea ubunge wa jimbo la Busega, Raphael Chegeni amesema kuwa atakiboresha kituo cha afya cha Nyashimo ili kiweze kuhudumia wananchi wa jimbo hilo kikamilifu
Akiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja ncha Nyahanga Kata ya Nyashimo, Chegeni alisema kuwa wananchi wamekuwa wakipata usumbufu kupata huduma katika kituo huku kikiwa na upungufu wa mkubwa wa dawa.
Chegeni alisema kuwa akipewa ridhaa kuongoza atahakikisha huduma za kijamii kama maji, afya na elimu zinaboreshwa ili wananchi wa jimbo hilo waweze kupata huduma za kijamii za uhakika.
“Ndugu zangu tumepanga kuboresha huduma za afya, elimu na maji ili wananchi waliopo katika jambo hili waweze kupata huduma za uhakika,na tumepanga kujenga shule ya kidato cha Tano na sita kwani wilaya ya Busega kwa ujumla haina shule hali ambayo inawalazimu wanafunzi kwenda wilaya jirani”Alisema Chegeni.
Alibainisha kuwa endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo ataboresha huduma za afya ili wananchi waweze kupatiwa huduma za uhakika hata wakina mama wanapoenda kujifungua waweze kujifungua salama
Mgombea udiwani kata ya Nyashimo Mickness Mahela alisema kuwa iwapo watapewa ridhaa ya kuongoza katika kata hiyo atahakikisha anaufufua mradi wa maji ambao umeshatelekezwa kwa muda mrefu.
Alisema kuwa mradi huo ndio mradi wa kuwakomboa wananchi wa wa kata hiyo kuondiokana na adha ya kukosa maji safi na kulazimika kufuata umbali mrefu maji ambayo sio safi na salama.
Mahela alibainisha kuwa amejipanga kuwasaidia wajasiliamali ambao wapo katika kata hiyo hasa vijana kuwapatia mikopo ambayo zitawawezesha kujiajili wenyewe ili kujiingizia kipato chao.
Awali akiongea katika mkutano huo aliyewahi kuwa makamu Mwenyekiti wa chama cha ushirika Nyanza ambaye pia ni kada wa ccm Silas Shipula alisema Mzee kingunge hana hekima kama wazee wengine ndio maana ccm haijateteleka kuondoka kwake.
Alisema kuwa mgombea uraisi wa ccm John Magufuli waliweza kumwajili katika ushirika huo na kumpatia fursa ya kwenda kusoma akiwa chini yao na kwamba anaweza kuwa raisi mwenye uchungu mkubwa na wananchi wake.
Wakiongea katika mkutano huo baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo alisema kuwa jimbo hilo linakabi;liwa na changamoto ya ukosefu wa maji na kero hiyo ikitatuliwa wanamini kuwa mbunge ajye anaweza kulitatua shida hiyo.
“Tunawaomba viongozi ambao watapika katika uchaguzi ujao waweze kufufua mradi wa maji ambao umeshachakaa na kuharibika kuuborsha ili uweze kuhudumia wananchi wote waliopo katika kata hiyo wanaoteseka kufuata maji ziwani umbali wa kilomita tatu”Alisema James Bangili.
Bagili pia alitaka vijana kupiga kura na kurudi nyumba kwa ajili ya kufanya shughuli nyingine kwa ukikaa mita 200 ukisubili kura ni kinyume kwani kila mgombea anawakala wake ndio analinda kura pale kituoni.
Alisema kuwa hata wagombea wanawajibu wa kuwaelimisha wafuasi wao wanapopiga kura warudi nyumba maana matokeo yanasomwa katika ofisi za msimamizi mkuu wa uchaguzi wa wilaya ambaye ni mkurugenzi wa Halmashauri.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni