Mkazi wa Kijiji cha Nyamatongo, wilayani Sengerema, Mwanza, akiwa amevaa kichwani mfano wa karatasi la kupigiwa kura lenye picha ya Mgombea urais wa Tganzania kupitia CCM, Dk John Magufuli na mgombea mwenza Samia Suluhu Hassan. Dk Magufuli alihutubia mkutano wa kampeni katika Kijiji hicho.
Dk Magufuli ameahidi kujenga viwanda vya kukamua juisi za mananasi yanayolimwa kwa wingi mkoani Geita ili kuongeza thamani ya zao hilo pamoja na kufufua viwanda vya pamba. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA, KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Wananchi wa Jimbo la Buchosa, wilayani Sengerema wakishangilia baada ya kumuona Dk Magufuli ambaye akizungumza nao aliahidi kujenga barabara kwa kiwango cha lami kutoka Sengerema hadi Nyahunga.
Mmoja wa wakazi wa Kasenyi akiwa amevaa kichwani karatasi la mfano la kuwapigia kura wagombea wa CCM, Dk Magufuli na Smia Suluhu Hassan wakati wa mkutano usio rasmi katika Kijiji hicho.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni