Nchi ya Myanmar imesema itasitisha
matumizi makubwa ya dola ya Marekani yanayofanywa na makampuni, ili
kuimarisha fedha yake ya Kyat.
Benki Kuu ya Taifa hilo imefuta
leseni za kufanya ubadilishaji fedha katika maeneo kadhaa ya
biashara, kuanzia ya hoteli za kitalii, migahawa, klabu za gofu
pamoja na hospitali.
Maamuzi hayo yanatokana na kuwepo
kwa ongezeko kubwa la mahitaji ya dola ya Marekani nchini Myanmar na
kusababisha kuwapo kwa kiwango kinachobadilika mara kwa mara cha soko
la kubadilishia fedha.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni