Familia ya Oscar Pistorius imeongea
kwa mara ya kwanza furaha waliyonayo baada ya mwanariadha huyo kutoka
gerezani baada ya kukaa mwaka mmoja kwa kosa la kumuua mpenzi wake
Reeva Steenkamp.
Mwanariadha huyo ambaye ni mlemavu
wa miguu yote miwili ametoka gerezani siku moja mapema na ataendelea
katumikia adhabu ya kifungo cha miaka mitano akiwa nyumbani kwao
Jijini Pretoria.
Inaaminika akiwa nyumbani ataweza
kuogelea bwawani, kumpumzika katika bustani, kuangalia TV pamoja na
kuweza kufanya mazoezi.
Nyumba atakayokuwa akikaa Pistorius akimalizia kifungo chake
Reeva Steenkamp akiwa na Oscar Pistorius
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni