Chama cha Liberals cha Canada
kimepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa wabunge, na kumaliza miaka
tisa ya utawala wa chama cha Conservative, kwa mujibu wa matokeo ya
awali.
Chama cha Liberals kinachoongozwa na
Justin Trudeau kinaongoza kwa kupata ushindi kwenye wilaya 185 za
uchaguzi.
Mtoto huyo wa aliyekuwa waziri mkuu
wa Canada marehemu Pierre Trudeau sasa anatarajiwa kuunda serikali ya
Canada, kwa mujibu ubashiri wa mtandao wa vyombo vya habari vya CBC
na CTV.
Waziri Mkuu aliyemadarakani kwa sasa
wa chama cha Conservative, Stephen Harper, ambaye chama chake
kinaongoza kwenye wilaya 103 za kupigia kura, amekubali kushindwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni