Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwanadi wagombea Ubunge wa jimbo la Chalinze,Mh Ridhiwan Kikwete (kulia) pamoja na Mh.Shukuru Kawambwa,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa wa shule ya msingi majengo wilayani humo jioni ya leo.
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema kugundulika kwa gesi ya Bagamoyo mkoani Pwani itasaidia kuimarisha uchumi na ujenzi wa viwanda nchini. Hayo ameyasema leo wilayani Bagamoyo katika mikutano yake ya kampeni iliyofanyika katika majimbo ya Chalinze na Bagamoyo, ambapo amesema gesi hiyo itasaidia ujenzi wa viwanda katika serikali take.

"Kwanza niwapongeze kwa kugundua gesi hapa Bagamoyo, tena imegunduliwa katika eneo la ruvu. Na hii itakuwa na manufaa kwa uchumi wa Taifa na kwa wananchi wa Pwani kwa ujumla.
"Gesi hii itasaidia sana ujenzi wa viwanda vya kisasa katika serikali ya Magufuli ya awamu ya tano. Tutajenga viwanda na tutatoa ajira za uhakika kwa vijana wa nchi hii pamoja na Tanzania yote," amesema Dk. Magufuli.
Wananchi wa Hedalu wakiwa wamefunga barabara wakimzuia mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli awasalimie na kumueleza shida zao ili akipata ridhaa ya kuwa Rais basi awasaidie kuyatatua matatizo hayo.
Wananch wakimshangilia Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli
Baadhi ya Wakazi wa Kiwangwa wakifuatilia Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipopita kuwasalimia akielekea wilayani Bagamoyo kwenye mkutano wa kampeni.PICHA NA MICHUZI JR-BAGAMOYO
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni