Kocha wa timu ya Taifa ya Oman ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer), Twalib Hilal jana ametoa msaada wa mipira 10 kwa ajii ya mchezo wa soka la ufukweni ambao umeanza kuwa maarufu nchni.
Twalib ambaye ni kocha na Mkufunzi wa FIFA wa soka la ufukweni alikabidhi mipira hiyo kwa Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine ikiwa ni sehemu ya mchango wake kwa maendeleo ya mchezo huo.
Kesho Jumamos tarehe 10 Oktoba, 2015 kocha Twalib atakutana na makocha, waamuzi wa mchezo wa ufukweni waliopo jijii Dar es salaam ili kubadilishana uzoefu saa 5 kamili asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni