Kiongozi
wa mapinduzi yaliyodumu kwa muda mfupi mwezi uliopita nchini Burkina
Faso, amefunguliwa mashtaka ya uhalifu yakiwemo ya kutishia usalama
wa taifa pamoja na ya mauaji.
Kiongozi
huyo mkuu wa kikosi cha kumlinda rais Jenerali Gilbert Diendere
anatarajiwa kukabiliwa na kesi yake katika mahakama ya kijeshi.
Baada
ya kushindwa kwa mapinduzi hayo rais Michel Kafando alirejeshwa
madarakani wiki mbili zilizopita, baada ya jeshi kuingilia kati
pamoja na viongozi wa mataifa ya Afrika Magharibi.
Kikosi
cha kulinda rais ambacho kilifanya mapinduzi hayo kitavunjwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni