Utafiti
uliofanywa umebaini kuwa nchi ya Uingereza inashika nafasi ya kwanza
kati ya mataifa 80 duniani ambayo yanaviwango bora vya mazingira ya
mtu kufariki dunia, yanayojali wagonjwa mahututi waliokwenye maumivu
makali pamoja na vikongwe.
Utafiti
huo wa ubora wa mazingira ya mtu kufariki dunia, uliofanywa na
Kitengo cha Uchumi na Intelejensia cha London, umeipatia Uingereza
asilimia 93.9 na kuwa taifa bora kwa mtu kufariki dunia, ikifuatiwa
na Australia, New Zealand, Ireland na Ubelgiji.
Katika
orodha hizo mataifa ya Uganda, Tanzania na Kenya yapo kwenye nafasi
za 20 za chini, wakati taifa la Bangladesh likishika nafasi ya mwisho
kwa kuwa na mazingira ambayo si rafiki kwa mtu kufariki dunia.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni