.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 4 Oktoba 2015

KOCHA JOSE MOURINHO AEPUKA KUTIMULIWA KIBARUA CHELSEA

Kocha Jose Mourinho ameepuka kutimuliwa kibarua baada ya kukutana na bodi ya timu ya Chelsea, kufuatia kufanya vibaya kwa timu hiyo na kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Southampton hapo jana.

Ilikuwa inahofiwa kuwa Mourinho atafukuzwa kazi ya kuinoa Chelsea baada ya kukubali kipigo cha sita katika msimu huu, ambapo yeye mwenyewe alionekana akimshawishi mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich kumfukuza kazi baada ya mchezo huo.

Badala yake bodi ya Chelsea imemtaka kocha Mourinho aendelee kukaa madarakani na kubadili hali ya matokeo mabaya ya timu hiyo, huku akiungwa mkono na bodi katika kufanya mabadiliko.
               Mourinho akiwashangaa wachezaji wa Chelsea wanavyovurunda uwanjani

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni