.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 4 Oktoba 2015

SERGIO AGUERO ATHIBITISHA NI MIONGONI MWA WACHEZAJI BORA KWA KUFUNGA TANO

Mshambuliaji nyota wa Manchester City striker Sergio Aguero amedhihirisha kuwa yeye ni miongoni mwa wachezaji bora waliopo katika Ligi Kuu ya Uingereza kwa wakati huu baada ya jana kucheka na nyavu mara tano.

Mchezaji huyo raia wa Argentina jana alifunga mabao hayo matano dhidi ya Newcastle United na kuisaidia timu yake kuibuka na uishindi wa mabao 6-1, katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Kwa kufunga magoli matano katika mchezo mmoja Aguero amefikia rekodi iliyowekwa na wachezaji Andy Cole, Alan Shearer, Jermain Defoe pamoja Dimitar Berbatov ambao nao walifunga idadi hiyo ya magoli katika Ligi Kuu ya Uingereza. 
 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni