.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 12 Oktoba 2015

LEWIS HAMILTON AMWAGIA RAIS PUTIN CHAMPAGNE AKISHEREHEKEA USHINDI

Dereva wa mbio za Langalanga Lewis Hamilton amesherehekea ushindi wake wa Sochi Grand Prix kwa kumwagia kidogo champagne rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa katika jukwaa la washindi.

Baada ya kupatiwa taji la ushindi wa mbio hizo zilizofanyika Urusi dereva Hamilton alianza kusherehekea kama ilivyo utamaduni wake kwa kutikisa na kumwaga champagne iliyokuwa kwenye chupa kubwa.

Rais Putin alimkabidhi Hamilton kombe la ushindi baada ya kuimba wimbo wa taifa, na wakati akiondoka Hamilton alianza kumwaga champagne kushangilia ushindi wake huo.
       Lewis Hamilton akishangilia kwa kumwaga champagne iliyomwagikia rais Putin
                       Mamodo pia ilibidi waoge champagne kama inavyoonekana hapa

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni