.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 14 Oktoba 2015

MAGAVANA WA AFRIKA WAKUTANA NA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA FEDHA LA KIMATAIFA BI. CHRISTINE LAGARDE

Magavana wa Afrika wakutana na Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa Bi. Christine Lagarde na Rais wa Kundi la Benki ya Dunia Dr. Jim Yong Kim kujadili namna ya kuchochea maendeleo na kuimarisha uchumi barani Afrika.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile wakisalimiana na Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa Bi. Christine Lagarde wakati akiingia kwenye ukumbi wa mkutano.
Katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa Bi. Christine Lagarde akinukuu hoja zilizokuwa zikijadiliwa katika mkutano huo.
Magavana wa Afrika wakiwa kwenye Mkutano wa majadiliano na Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa Bi. Christine Lagarde na Rais wa Kundi la Benki ya Dunia Dr. Jim Yong Kim nchini Peru – Lima.
Wa pili kulia ni Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile akifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye mkutano. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi Benki Kuu ya Tanzania Dr. Joseph Masawe.
Ujumbe wa Tanzania wakiwa kwenye mkutano wakujadili namna ya kuimarisha uchumi na kuchoche maendeleo Barani Afrika. Kutoka kushoto ni Kamishna Idara ya Sera Bw. Bedason Shallanda, Mhasibu Mkuu Msaidizi Bw. Ishmael Kasekwa, John Mavura mchumi Wizara ya Fedha na Bw. Patrick Pima mchumi Wizara ya Fedha.

                                                                                                 Imetolewa na
                                                                                Msemaji wa Wizara ya Fedha
                                                                                        Bi. Ingiahedi Mduma
                                                                                                   13/10/2015

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni