Mshambuliaji
wa Stoke City Mame Biram Diouf amefahamishwa kuwa mama yake mzazi ni
miongoni mwa mahujaji waliokufa katika tukio la msongamano katika mji
mtakatifu wa Mekka, mwezi uliopita.
Tukio
hilo lilitokea katika siku ya mwisho ya Hija Septemba 24 na kuuwa
mahujaji zaidi ya 700, kutokana na kukanyagana katika mji wa Mina.
Mama
wa mchezaji soka Diouf, aitwae Gnilane, alikuwa anahudhuria tukio
muhimu la kiimani la kumpiga shetani mawe, ambapo mahujaji hutupa
mawe kwenye nguzo kubwa katika kukamilisha ibada ya Hija.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni