Mshambuliaji
Wayne Rooney huenda akakosa kuichezea Uingereza katika mchezo wa
kuwaniakufuzu michuano ya Euro 2016 dhidi ya Estonia Ijumaa huku naye
John Stones akiondolewa kikosini kutokana na kuwa majeruhi.
Mshambuliaji
huyo wa Manchester United na Kapteni wa Uingereza alionekana akiwa
amekaa wakati kikosi hicho cha Roy Hodgson kikifanya mazoezi katika
dimba la St George's Park hapo jana huku Danny Ings, akiitwa kwa mara
ya kwanza.
Wayne
Rooney na Jonjo Shelvey, ambaye ni majeruhi wataendelea kuwa chini ya
uangalizi timu ya madaktari wa Uingereza, ingawa wawili hao
kunauwezekano kutoingia dimbani Ijumaa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni