.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 22 Oktoba 2015

MGOMBEA MWENZA WA URAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA WANAWAKE WA PEMBA

Naibu Katibu Mkuu wa UWT, Salama Aboud akielezea umuhimu wa wanawake wa Tanzania, kukiunga mkono chama cha mapinduzi, ili kuzidi kuimarisha uchumi wao, kwenye mkutano wa kampeni uliohutubiwa na Mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: Samia Suluhu Hassan, uliofanyika skuli ya sekondari ya Fidel Castro Chake chake Pemba.
 Katibu wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba, Khadiji Nassor Abdi, akizunguma kwenye mkutano wa kampeni, uliohutubiwa na Mgombea mwenza wa urais, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: Samia Suluhu Hassan, uliofanyika skuli ya sekondari ya Fidel Castro Chake chake Pemba.
Mgombea Mwenzawa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Mhe: Samia Suluhu Hassan, akizungumza na wanawake wa chama hicho wa wilaya nne za Pemba, kwenye mkutano uliofanyika skuli ya sekondari ya Fidel Casto wilaya ya Chake chake.
Wahamasishaji wakiongozwa Mhe: Faida Mohamed Bakari (kulia), wakiimba wimbo maalumu kwenye mkutano wa kampeni uliohutubiwa na Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: Samia Suluhu Hassan, uliofanyika skuli ya sekondari ya Fidel Castro Chake chake Pemba
Wanawake wa CCM wa wilaya nne za Pemba, wakiwa na furaha kubwa, mara baada ya Mgombea Mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani kwa tiketi ya chama hicho Mhe: Samia Suluhu Hassan, alipowasili kwenye ukumbi wa skuli ya sekondari ya Fidel Castro wilaya ya Chake chake, kumuombea kura mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: John Pombe Magufuli. Kwa hisani ya ZanziNews

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni