.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 8 Oktoba 2015

MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KWA TIKETI YA CCM, DK. SHEIN AWATAMBULISHA WAGOMBEA UBUNGE NA UWAKILISHI WA WILAYA YA AMANI UNGUJA KICHAMA

Wasanii wa Kikundi cha Big Star wakitowa burudani kwa wimbo maalum wa Kapeni wakati wa mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein.zilizofanyika katika viwanja vya mpira vya Urafiki mikunguni Unguja
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa katika viwanja vya mkutano wa mkgombea Urais wa Zanzibar kwa kupitia CCM wakishangilia kwa kupeperusha bendera za Chama wakati wa mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya mpira urafiki mikunguni Zanzibar.
Mwanachama wa CCM akishangilia kwa kuonesha picha ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Mhe Borafya Silima akiwahutubia wananchi katika viwanja vya urafiki mikunguni akielezea mafanikio ya CCM yaliopatika kutokana Ilani ya Uchaguzi ya miaka mitano ya Dk Ali Mohamed Shein, wakati wa mkutano wa Mgombea Urais wa Zanzibar uliofanyika katika viwanja hivyo.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi Seif Aki Iddi wakiwa katika jukwaa kuu wakati wa mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika Jimbo la Shaurimoyo Wilaya ya Mjini Amani Kichama katika viwanja vya mpira vya urafiki mikunguni.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mhe. Haroun Ali Suleima akiwahutubia wananchi na kuzungumzia Ajira wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya CCM Uliofanyika katika Jimbo la Shaurimoyo Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Kwahani Mhe Dk Hussein Ali Hassan Mwinyi akiwahutubia Wanancxhi katika mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar na kuelezea Ajira kwa Vijana katika Serikali ya Muungano wakati wa mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya mipira vya urafiki Zanzibar.
Wanachama wa CCM wakifuatilia mkutano wa Mgombea Urais wa Zanzibar katika uwanja wa mpira wa urafiki mikunguni Zanzibar uliohutubiwa na Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein.
Balozi Amina Salim Ali akiwahutubia Wananchi wakati wa Mkutano wa Kampeni ya mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, uliofanyika katika viwanja vya urafiki na kutowa Salamu za Umoja wa Mataifa kuhusiana na Zanzibar kupiga hatua katika suala la Ajira kwa Vijana.
Mjumbea wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia wananchi na kuwataka Vijana kupamba maskani zao ili kusherehekea ushindi wa CCM katika uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, na kuelezea jinsi ya mafanikio ya Ilani ya CCM kwa kipindi cha miaka mitano ya Uongozi wa Dk Shein, ilivyosimamia maendeleo katika sekta mbalimbali za Uchumi wa Zanzibar. na kuwataka kuipigia Kura CCM.chini ya Uongozi wake Dk.Ali Mohamed Shein.
















Hakuna maoni :

Chapisha Maoni