Umoja
wa Ulaya unaanza operesheni mpya za kudhibiti boti zinazovusha
wahamiaji kimagendo kukatiza bahari ya Mediterranean.
Chini
ya Operesheni hiyo iitwayo Sophia, boti za vikosi vya wanamaji
zitaruhusiwa kuingia, kufanya upekuzi, kuzikamata na kuzitimua boti
zinazohisiwa kubeba wahamiaji.
Hadi
sasa Umoja wa Ulaya umejikita katika uangalizi na operesheni za
uokoaji wahamiaji ambao boti zao huzama mara kwa mara kutokana na
kuwa duni na zenye kujaza mno watu.
Takwimu
zinaonyesha zaidi ya wahamiaji na wakimbizi 130,000 wamekatiza Ulaya
wakitokea pwani ya kaskazini mwa Afrika, huku wengine zaidi ya 2,700
wakifa maji.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni