Njemba mmoja mkazi wa mji wa Zhengzhou, nchini China, amepewa cheo cha Mfalme wa Pilipili kutokana na tabia yake ya kula kilo mbili na nusu za pilipili ya unga kila siku. Kinyeme na watu wengine ambao huanza siku yao kwa kupiga mswaki, njemba huyo aitwaye Li Yongzhi, yeye huanza siku yake kwa kubwia kikombe kimoja cha pilipili ya unga huku akisukumia na kikombe cha maji yenye pilipili.
Na wakati watu wengine wakidhani kuwa anatumia nguvu za giza kufanya mambo hayo, Li ambaye chai yake hunogeshwa na funda jingine la kama robo kilo ya pilipili, amesema ameweza kula kiasi hicho cha pilipili kutokana na mapenzi yake kwa chachandu hiyo.
Amesema alianza kupenda kula pilipili kila alipohisi chakula nachokula hakina viungo vya kumchangamsha na taratibu akaanza kuipenda pilipili kiasi cha kumfanya aanze kulima robo heka ya shamba la pilipili na sasa anakula kiasi cha kilo mbili na nusu kwa siku huku akitembea na mfuko wa pilipili ya unga.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni