Mzee mstaafu raia wa Uingereza
aliyekamatwa nchini Saudi Arabia akiwa na mvinyo wakutengeneza
nyumbani anakabiliwa na adhabu ya kuchapwa viboko 360, jambo ambalo
familia yake imesema litamsababishia kifo.
Mzee huyo Karl Andree, mwenye umri
wa miaka 74, ameshatumikia adhabu ya zaidi ya mwaka mmoja jela tangu
alipokamatwa na polisi wa Saudi Arabia wanaofuata taratibu za dini ya
Kiislam.
Binti wa mzeee Andree, Kirsten
Piroth ameliambia shirika la habari la BBC, kuwa baba yake ambaye
anasumbuliwa na tatizo la aina tatu za saratani hatoweza kumudu
adhabu hiyo ya kuchapwa viboko 360.
Ofisi ya Uingereza ya Mambo ya Nje
imesema kuwa inajaribu kushughulikia suala la mzee huyo ili aachiwe
huru mara moja.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni