Mwalimu mmoja wa kike nchini Kenya
ametekwa jana katika kambi ya Hagadera huko Dadaad katika kaunti ya
Garissa na watu wanaoshukiwa kuwa ni wapiganaji wa kundi la
Al-Shabaab la nchini Somalia.
Afisa wa jeshi la polisi OCDP
Raphael Kimilu amesema kuwa bado hawajafanikiwa kumpata mwalimu huyo
ambaye ni muajiriwa wa Shirika lisilolakiserikali la Trust
International.
OCDP Kimilu amesema amesambaza
maafisa polisi katika mpaka wa Kenya na Somalia ambapo inaaminika
wapiganaji hao wa Al-Shabaab wanamshikilia mwalimu huyo aitwae Judy
Mutua.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni