Rais wa Argentina, Bi. Cristina
Fernandez pamoja na Shirika la Kimataifa la Amnesty wametaka haki
kutendeka kufuatia kifo cha mwanaharakati aliyejibadilisha jinsia.
Mwanaharakati huyo Diana Sacayan,
ambaye ni maarufu kwa harakati za haki za mashoga na wasagaji
alikutwa akiwa amekufa Jijini Buenos Aires ndani ya ghorofa siku ya
jumanne.
Hili ni tukio la tatu la ukatili
uliosababisha mauaji dhidi ya watu waliobadili jinsia tangu katika
mwezi uliopita.
Mataifa ya Latini Aamerika yamekuwa
na matukio mengi ya mauaji ya watu waliobadili jinsia duniani.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni