Aliyekuwa rais wa Benin, Mathieu
Kerekou, ambaye alipongezwa kwa kuleta demokrasia ya vyama vingi
nchini Afrika amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82.
Bw. Kerekou alikuwa rais kwa mihula
miwili tofauti ya miaka 30, kwa mara ya kwanza alikuwa mkuu wa nchi
wakati wa sera za Marxist katika mwaka 1972.
Hata hivyo alikubali wazo la kuwa na
mfumo wa vyama vingi na kufanya uchaguzi ambao alikuja kupoteza
madaraka mwaka 1991.
Marehemu Kerekou alikuwa rais wa
kwanza wa mataifa ya Afrika ya Magharibi kukubali kushindwa katika
uchaguzi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni