Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja leo jijini Dar es Salaam. |
Hapa ni wakati wa kugonganisha glasi za mvinyo kutakiana afya njema na utendaji bora...! |
Alisema maofisa waandamizi wa kampuni hiyo watashiriki moja kwa moja katika zoezi hilo la kutoa huduma pamoja na kuwatembelea wateja kupata maoni yao na pia kutoa shukrani kwa wao kukubali kuhudumiwa na kampuni hiyo ya simu ya kizalendo nchini Tanzania.
"...Mbali na kutoa huduma zetu katika matawi mbalimbali katika kipindi hiki maofisa waandamizi wa TTCL watawatembelea wateja moja kwa moja katika ofisi zao au majumbani kwa ajili ya kuwasikiliza na pia kupokea naoni yao," alisema Leonard akizungumza katika hafla hiyo.
Katika uzinduzi wa hafla hiyo TTCL ilitoa zawadi kwa wateja watano wa mwanzo waliofika katika vituo vya huduma kwa wateja leo asubuhi kuhudumiwa na kampuni hiyo pamoja na kuwazawadia maofisa wa TTCL waliofanya vizuri zaidi katika idara ya huduma kwa wateja ya kampuni hiyo, ikiwa ni motisha ya kuchochea utendaji bora zaidi.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni