Supamaketi ya Uchumi imetangaza
kujiondoa kufanya biashara katika nchi za Tanzania na Uganda katika
kusitisha upotevu zaidi wa fedha.
Mtendaji Mkuu wa Uchumi Supamaketi
Bw. Julius Kipng'etich, amesema bodi ya kampuni hiyo imeamua kufunga
maduka yake yote yakikanda ili kuimarisha shughuli zake za nchini
Kenya.
Bw. Kipng’etich amesema Supamaketi
zao za Tanzania na Uganda ni asilimia 4.7 tu ya maduka yake yote
lakini zinagharimu asilimia 25 za gharama za uendeshaji.
Amesema maduka ya Uchumi ya mataifa
hayo mawili ya Afrika Mashariki hayajaingiza faida kwa miaka mitano
iliyopita, jambo ambalo linaonyesha yalikuwa yakinyonya fedha za
makao makuu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni