Baraza la Mawaziri la Israeli
limeliagiza jeshi la polisi kufunga sehemu ya Jerusalem katika
jaribio la kusitisha wimbi la mashambulizi mabaya.
Baada ya mkutano wa dharura, baraza
la mawaziri limesema wanajeshi pia watapelekwa kusaidiana na polisi
katika baadhi ya maeneo.
Uamuzi huo umekuja baada ya polisi
kusema kuwa Waisraili watatu wameuwawa na zaidi ya 20 wamejeruhiwa
kwa risasi pamoja na kuchomwa visu Jerusalem na kati kati ya Israeli.
Washambuliaji wawili waliotambuliwa
kuwa ni Wapalestina wameuwawa kwa risasi na polisi Jijini Jerusalem.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni