Marekani na Urusi zinafanya
mazungumzo juu ya usalama wa anga Syria baada ya kubainika kuwa ndege
zake zinazofanya mashambulizi katika nchi hiyo zilikaribiana kwa
umbali wa takribani kiliomita 15 siku ya Jumamosi.
Ndege hizo zilikuwa katika umbali wa
kuonana wa kilomita 15 hadi 30, Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya
Marekani amewaambia waandishi wa habari Jijini Washington DC.
Mazungumzo hayo ya mataifa hayo
mawili yatakuwa ni ya mzungumko wa tatu, katika kujaribu kuepusha
kuibuka kwa mapigano ya bahati mbaya baina yao nchini Syria. Waziri
wa Ulinzi wa Marekani Ash Carter amesema anatarajia makubaliano
kufikiwa mapema.
Urusi ilianza kampeni za
mashambulizi ya anga nchini Syria Septemba 30 ikisema inawalenga
Wapiganaji wa Dola ya Kiislam (IS), baada ya kuombwa kusaidia jeshi
la nchi hiyo na rais wa Syria Bashar al-Assad.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni