Mchezaji nyota wa mpira wa kikapu wa
NBA nchini Marekani Lamar Odom anapigania maisha yake baada ya
kupoteza fahamu na moyo kushindwa kufanya kazi alipomtembelea kaka
yake huko Nevada baada ya sherehe za mwisho wa wiki na kunywa vidonge
mbadala wa viagra.
Mchezaji huyo wa kulipwa wa mpira wa
kikapu alikuwa kwenye nyumba ya Dennis Hof, iliyopo Pahrump wakati
tukio hilo likitokea jumanne mchana ikiwa ni siku kadhaa kupita tangu
afike hapo jumamosi.
Mke wake wa zamani Khloe Kardashian
pamoja na dada yake Kim na mama yao Kris Jenner wameonekana wakiwa
kando ya kitanda alicholala Odom, na mwakilishi wa Khloe ameitwa
kukusanya kila kitu cha Odom.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni