.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 15 Oktoba 2015

VIONGOZI WA JUMUIYA YA ULAYA KUJADILI MGOGORO WA WAHAMIAJI

Viongozi wa Ulaya watajadili hatua za kurahisisha mgogoro wa wahamiaji, huku Uturuki ikiwa ndio gumzo katika jitihada hizo Jijini Brussels.

Karibu watu laki 6 wameingia nchi za Umoja wa Ulaya kwa kutumia bahari hadi sasa katika kipindi cha mwaka huu.

Uturuki inawahamiaji milioni 2, wengi wao wakiwa wamekimbia vita katika nchi jirani za Syria.

Kuelekea mkutano huo Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amehimiza umuhimu wa kuwepo kwa jitihada za pamoja kukabiliana na mgogoro wa wahamiaji na kusema Uturuki inajukumu muhimu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni