Wananchi wa Misri wameshiriki kupiga
kura hii leo katika zoezi la kwanza la upigaji kura wa kuwachagua
wabunge, ambalo lilicheleweshwa kwa muda mrefu.
Huu ni uchaguzi wa kwanza wa
wabunge, baada ya bunge lililopita kuvunjwa na uamuzi wa mahakama
uliotolewa mwaka 2012.
Mamlaka za nchini Misri zimesema
uchaguzi huo ni hatua ya mwisho ya mpito kuelekea katika Demokrasia.
Hata hivyo wakosoaji wa mambo
wamesema wagombea wengi wa ubunge ni watu wanaomuunga mkono rais
Abdul Fattah al-Sisi hivyo bunge jipya litaendelea kumpa madaraka
rais huyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni