Nyumba nyingi zimeangushwa chini,
nguzo za umeme kuanguka na maelfu ya watu wamekimbia nyumba zao
kufuatia kimbunga kiitwacho Koppu kulikumba eneo la kaskazini mwa
Philippines.
Kimbunga hicho kikubwa kinachoenda
taratibu kimesababisha maporomoka ya ardhi karibu na mji wa Casiguran
kwenye kisiwa cha Luzon leo asubuhi.
Kimbunga Koppu kimekusanya upepe
wenye kasi ya kilimita 200 kwa saa na kuchangia ongezeko la maji
baharini la urefu wa mita 4.
Siku tatu za mvua za pia
zimetabiriwa kufuata jambo ambalo litapelekea kuwepo kwa mafuriko
makubwa pamoja na uwezekano wa kutokea maporomoko ya ardhi nchini
Philippines.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni