Mgombea anayeongoza katika
kinyang'anyiro cha umeya wa Jiji la Cologne amechomwa kisu shingoni
na mwanaume mmoja anayedaiwa kuchukizwa na sera za nchi hiyo kuhusu
wakimbizi.
Bi. Henriette Reker ambaye ni
mgombea binafsi anayeungwa mkono na Kansela Angela Merkel wa chama
cha CDU, amejeruhiwa vibaya pamoja na msaidizi wake. Watu wengine
watatu wamepata majeraha madogo.
Polisi wanamshikilia mwanaume huyo
Mjerumani mwenye umri wa miaka 44, mkazi wa Cologne kwa kuhusika na
tukio hilo la kumchoma kisu Bi. Reker, ambaye hali yake inaelezwa
kuwa bado si nzuri sana.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni