Watoto wawili wamebakwa katika Jiji
la Delhi nchini India na kumfanya waziri kiongozi wa jiji hilo kutoa
shutuma kali.
Waziri huyo Arvind Kejriwal
ameishutumu serikali pamoja na polisi kwa kutofanya jitihada za
kutosha kuwalinda watoto katika Jiji la Delhi.
Matukio hayo ya kubakwa watoto
yamejitokeza ikiwa ni wiki moja tu kupita tangu kubakwa mtoto wakike
wa miaka minne Jijini Delhi.
Miaka miwili iliyopita India
iliongeza makali kuhusiana na makosa ya ukatili wa kingono, baada ya
genge moja la watu wakatili kumbaka na kumuua mwanafunzi wa kike.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni