Washambuliaji wa kujitoa mhanga
wameshambulia soko la samaki pamoja na kambi ya wakimbizi katika mji
wa Baga Sola magharibi mwa Chad, na kuuwa watu 30.
Maafisa wa nchi hiyo wamesema zaidi
ya watu 50, wanatibiwa katika hospitali ya mji huo ambao upo kwenye
fukwe ya ziwa Chad.
Kambi hiyo ipo nje ya mji Baga Sola
ni makazi ya makumi kwa maelfu ya Wanigeria ambao walikimbia
mashambulizi ya Boko Haram.
Nchi ya Chad ni mwenyeji wa vikosi
vya kikanda vinavyokabiliana na wapiganaji wa Boko Haram nchini
Nigeria.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni