.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 11 Oktoba 2015

WALES WATINGA EURO 2016 LICHA YA KUPATA KIPIGO KUTOKA KWA BOSNIA

Timu ya taifa ya Wales ikiongozwa vyema na nyota wao Gareth Bale imefanikiwa kutinga michuano ya Euro 2016 licha ya kikosi chao kinachonolewa na kocha Chris Coleman kufungwa jana usiku.

Wales imefanikiwa kufuzu kuingia katika michuano hiyo jana usiku kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1958, hata baada ya kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Bosnia katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Bilino Polje.

Katika mchezo huo Bosnia iliandika bao la kwanza kupitia kwa Milan Djuric kwa kichwa cha kunyanyua mpira juu na kumpita Wayne Hennessy, ambapo Vedad Ibisevic aliipachikia Bosnia bao la pili.
                   Furaha ya kufuzu Euro 2016, Bale na wenzake wakitereza uwanjani
                              Kocha Chris Coleman akibebwa juu juu na wachezaji wa Wales

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni