Waziri Mkuu wa Isareli Bw. Benjamin
Netanyahu amemsihi kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas kufanya
mazungumzo ya kutuliza kuibuka kwa ghasia za hivi karibuni.
Bw. Netanyahu amesema anamatumaini
mkutano huo utakuwa na manufaa mno katika kutuliza ghasia hizo.
Aidha, Netanyahu ametetea hatua ya
kuweka ulinzi makali Jerusalem kufuatia wimbi la matukio ya
mashambulizi ya kutumia kisu yanayofanywa na Wapalestina.
Matukio hayo ya karibia kila siku
yameuwa Waisraeli saba na makumi kujeruhiwa kwa siku kadhaa
zilizopita.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni