Mgombea wa Ubunge Viti Maalum katika
jimbo la Kilombero kwa tiketi ya Chadema Amy Pascience amefungua
chini ya hati ya haraka sana shauri namba 37 la mwaka 2015 katika
Mahakama Kuu ya Tanzania kuomba mahakama itoe tafsiri sahihi ya
kifungu namba 104 (1) cha sheria ya uchaguzi Tanzania itamke iwapo
wapiga kura na watu wengine wenye shauku wanaruhusiwa au la kukaa
kwa utulivu umbali wa mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura ama cha
kufanyia majumuisho ya kura.
Katika shauri hilo Mahakama kuu pia
imeombwa kutamka iwapo ni halali kwa rais wa nchi kutoa matamko
aliyoyatoa kwa namna ya katazo kwa wapiga kura ama raia wenye shauku
kukaa kwa utulivu umbali wa mita 200 kutoka katika kituo cha kupigia
kura ama cha kufanya majumuisho kungojea matokeo.
Akizungumzia juu ya shauri hilo
lililofunguliwa leo na wakili Peter Kibatala kwa niaba ya mteja wake
huyo, amesema aidha, katika shauri Mahakama Kuu imeombwa itamke iwapo
rais ana mamlaka hayo kisheria kwa kuzingatia sheria ya uchaguzi
Tanzania.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni