Usiku mzuri wa jana kwa klabu ya
Tottenham katika dimba la White Hart Lane uliisha kwa shari baina ya
Andros Townsend ambaye alionekana akikwaruzana na kocha wa viungo
Nathan Gardiner baada ya kumalizika mchezo huo.
Winga huyo wa kimataifa wa timu ya
taifa ya Uingereza, ambaye alikuwa ni mchezaji wa akiba ambaye
hakutumika wakati timu yake ya Tottenham kuibuka na ushindi wa mabao
3-1 dhidi ya Aston Villa.
Townsend alisugua benchi na kujikuta
akiishia kuangalia kocha Mauricio Pochettino akimuingiza kiungo kinda
Josh Onomah, kutoka benchi.
Andros Townsend akisukumana na kocha wa viungo Nathan Gardiner
Andros Townsend akijibizana na kocha wa viungo Nathan Gardiner



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni