Kundi la wapiganaji wa Kiislam la
Boko Haram limetoa picha zinazoonyesha wakiwa na kiwanda cha
kutengeneza makombora ya roketi kaskazini-mashariki mwa Nigeria.
Kundi hilo limekuwa likitumia
makombora ya roketi katika mashambulizi yake siku za nyuma na
Wanaigeria wengi walikuwa wakihoji Boko Haram wanaizitoa wapi silaha
hiyo..
Picha hizo zinaashiria kuwa
wapiganaji wa Boko Haram wanaujuzi wa kutengeneza makombora
ya roketi katika kiwanda hicho.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni