Vipimo vitafanywa kubaini kwanini
aridhi imepasuka na kumeza magari 12 huko Mississippi nchini Marekani
katika eneo la maegesho ya magari kwenye hoteli moja.
Shimo hilo la kupasuka ardhi lenye
urefu wa mita 120 na upana wa mita 11 lilifunguka jumamosi huko
Meridian, karibu na jimbo la Alabama.
Eneo hilo lilipata mvua kubwa kwa
wiki mbili zilizopita, gazeti la Meridian Star limeandika. Hakuna mtu
aliyejeruhiwa katika tukio hilo.
Magari yakiwa yametumbukia aridhini baada ya ardhi kupasuka
Gari likiwa limenusurika kidogo kutumbukia baada ya ardhi kupasuka



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni