.
.
.
.
.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga
|
TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.
mbani
NYUMBANI
HABARI
SIASA
MICHEZO
BURUDANI
TABASAMU
KIMATAIFA
Ijumaa, 6 Novemba 2015
BALOZI MULAMULA AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA BURUNDI
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe, walikutana leo na kufanya mazungumzo hapa Wizarani, Mazungumzo yao yalijikita katika kukuza na kuimarisha Ushirikiano kati ya Tanzania na Burundi katika sekta mbalimbali
Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Rajab Gamah (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Samweli Shelukindo (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Mindi Kasiga nao wakifuatilia kwa makini mazungumzo yaliyo kuwa yakiendelea kati ya Baozi Mulamula na Waziri Nyamwite (hawapo pichani)
Waziri Nyamitwe hakusita kuelezea furaha yake ya kupata fursa ya kuhudhuria sherehe za Uapisho wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli hapo jana.
Mazungumzo yakiendelea kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Mulamula (wa tatu kushoto) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi (wa pili kutoka kushoto), na wakwanza kushoto ni Balozi wa Burundi nchini Mhe. Issa Ntambuka.
Picha na Reginald Philip
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni
Chapisho Jipya
Taarifa za zamani
Nyumbani
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni ( Atom )
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni