Bondia Anthony Crolla ametimiza
ndoto yake ya kutwaa taji la dunia la uzani wa lightweight la WBA,
baada ya kumdunda Darleys Perez.
Crolla alimpiga kwa KO mpinzani wake
katika raundi ya tano, kwa kumpiga ngumi ya kwenye mwili iliyompeleka
chini.
Raia huyo wa Uingereza ameonekana
kupona vyema jeraha la fuvu la kichwa alilopata wakati akiwakimbiza
wezi katika nyumba ya jirani wake huko Oldham.
Anthony Crolla akimtwanga ngumi Darleys Perez
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni