.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 22 Novemba 2015

LIVERPOOL YACHARUKA NA KUICHAKAZA MAN CITY NYUMBANI MABAO 4-1

Timu ya Liverpool imeichakaza Manchester City na kufuta matumaini yake ya kurejea kuongoza Ligi Kuu ya Uingereza, baada ya kupata ushindi wa mabao 4-1 katika dimba la Etihad hali inayoashiria kuimarika ikiwa chini ya Jurgen Klopp.

Kikosi hicho cha Klopp kiliwapeleka puta wenyeji Manchester City ambapo katika kipindi cha kwanza tu tayari walifunga mabao 3-0, yaliyofungwa na Eliaquim Mangala aliyejifunga, na kufuatiwa na bao murwa la Philippe Coutinho pamoja na bao la Roberto Firmino.

Sergio Aguero aliipa matumaini Manchester City baada ya kufunga goli moja, hata hivyo beki ya timu hiyo ilionekana kuwa kichochoro baada ya kuumian kapteni wao Vincent Kompany, na Martin Skrtel alifunga kitabu kwa kupachika bao la nne.
                                                Mshambuliaji Roberto Firmino akipachika bao
Nayo Chelsea iliambulia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Norwich, kupitia kwa mchezaji wake Diego Costa. Matokeo mengine ya ligi hiyo jana ni Watford 1 - 2 Man Utd, Everton 4 - 0 Aston Villa, Newcastle 0 - 3 Leicester, Southampton 0 - 1 Stoke, Swansea 2 - 2 Bournemouthna West Brom 2 - 1 Arsenal.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni