Barcelona imefanikiwa kuongoza Ligi
Kuu ya Hispania (La Liga) kwa tofauti ya pointi sita, wakati Luis
Suarez akicheka na nyavu mara mbili katika kipigo cha mabao 4-0 dhidi
ya mahasimu wao Real Madrid kwenye dimba la Bernabeu.
Wageni Barcelona waliweza kuudhibiti
mchezo wao huo maarufu kama El Clasico kwa muda wote, ambapo Luis
Suarez alikuwa wakwanza kufunga bao kwa shuti la yati 16, kabla ya
Neymar naye kutumbukiza bao.
Andres Iniesta alipachika bao la
pili baada ya mapumziko na kisha Suarez akafunga karamu ya mabao,
kabla ya Isco hajatolewa nje kwa kucheza rafu.
Matokeo mengine ya Ligi Kuu ya
Hispania hapo jana yalikuwa Real Sociedad 2 - 0 Sevilla, Espanyol
2 - 0 Málaga, Valencia 1 - 1 Las Palmas na Deportivo de La Coruña
2 - 0 Celta de Vigo.
Neymar akiruka juu kushangilia bao lake alilofunga
Suarez akitikisa nyavu huku Messi kushoto akiangalia
Cristiano Ronaldo akionyesha kukasirika baada ya kukosa goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni