Chama cha National League for
Democracy kinachoongozwa na Bi. Aung San Suu Kyi kimepata ushindi
mkubwa wa kihistoria katika uchaguzi wa ubunge nchini Myanmar.
Wakati matokeo ya asilimia 80 ya
viti vya ubunge yakitangazwa chama hicho cha Bi. Suu Kyi kimetwaa
viti vya ubunge zaidi ya theluthi mbili na kuwa na mamlaka ya
kuchagua rais na kumaliza muongo mmoja wa utawala unaoungwa mkono na
jeshi.
Hata hivyo robo ya viti vya ubunge
vimetengwa kwa jeshi, jambo ambalo linamaanisha kwamba jeshi bado
litakuwa na ushawishi mkubwa. Chini ya Katiba ya sasa Bi. Suu Kyi
hawezi kuwa rais.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni