.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 13 Novemba 2015

RAIA WA DENMRAK AKAMATWA KWA KUKEKETA WANAWAKE AFRIKA KUSINI

Mwanaume mmoja raia wa Denmark anayetuhumiwa nchini Afrika Kusini kwa kosa la kukeketa wanawake, amekanusha shtaka la kuhusika na kifo cha mke wake, ambaye alikuwa ni shahidi mkuu wa kesi yake.

Mwezi Septemba mwaka huu polisi nchini Afrika Kusini walibaini mifuko 21, iliyokuwa na vijinyama vilivyokeketwa kutoka kwa wanawake hao, pamoja na vifaa vya upasuaji kwenye friji inayomilikiwa na mtuhumiwa huyo Peter Frederiksen, mwenye umri wa miaka 63.

Wiki kadhaa baadae mke wake ambaye alikuwa ndiye shahidi mkuu wa upande wa serikali alipingwa risasi na kufa akiwa nchini Lesotho.

Mwendesha mashtaka Amanda Bester ameiambia mahakama kuwa mke wa Bw. Frederiksen, Anna Matseliso Molise, 28, aliuwawa kwa sababu anajua mamombo mengi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni