Mabalozi wa nchi muhimu za magharibi
nchini Kenya wameonyeshwa kusikitishwa na matukio ya mfululizo ya
kashfa za rushwa yaliyoikumba serikali ya Jubilee na kusema
yanadhoofisha uchumi na usalama.
Katika taarifa yao ya pamoja
mabalozi hao wa mataifa 11 ya magharibi, ambao ni miongoni mwa
wafadhili wakubwa wa Kenya wametishia kuwawekea vikwazo vya
kutokusafiri nje maafisa wa serikali waliohusishwa na vitendo vya
rushwa.
Baada ya kutembelea Tume ya Maadili
na Kukabiliana na Rushwa (EACC), wawakilishi hao wa mataifa ya kigeni
Kenya wamesema hawawezi kukaa na kuangalia tu uongozi wa serikali ya
rais Uhuru Kenyatta ukikithiri kwa rushwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni