Watu wapatao 37 wameuwawa na wengine
181 wamejeruhiwa katika matukio mawili ya mabomu ya kujitoa mhanga
katika makazi ya watu katika Jiji la Beirut nchini Lebanon.
Watu hao waliojitoa mhanga
wamejilipua katika barabara yenye shughuli nyingi katika kitongoji
cha Burj al-Barajneh ambacho ni ngome kuu ya Waislamu wa Dhehenu la
Shia wa kundi la Hezbollah.
Kundi la jihadi la Sunni la Dola ya
Kiislama (IS) limedai kuhusika na tukio hilo, hata hivyo hakuna
taasisi huru iliyothibitisha madai hayo. Tukio hilo ni baya kuwahi
kutokea tangu machafuko yaliyomalizika miaka 25 iliyopita.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni