Golikipa wa timu ya Chelsea, Asmir
Begovic, amesema kocha Jose Mourinho anaungwa mkono na wachezaji wake
kuwa ni mtu sahihi anayeweza kubadili hali ya vipigo inayoendelea
kuikabili timu hiyo.
Chelsea imepoteza mechi ya jana kwa
kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Stoke City, ikiwa ni kipigo
cha tatu mfululizo na kujikuta katika nafasi ya 16 katika msimamo wa
Ligi Kuu ya Uingereza.
Katika mchezo huo Mourinho alikosa
kuwepo uwanjani kufuatia adhabu ya chama cha Soka Uingereza kumfungia
kutohudhuria mechi moja, badala yake alishuhudia mchezo huo akiwa
hotelini.
Mashabiki wa Chelsea wakibebe picha ya Mourinho kudhihaki kuwa yupo uwanjani.
MAN U YAUONA MWEZI....
Kinda Jesse Lingard amefunga goli
lake la kwanza katika Ligi Kuu ya Uingereza na kuisaidia Manchester
United kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya West Brom katika mchezo
uliochezwa kwenye dimba la Old Traffiord.
Jesse Lingard alipachika bao hilo
zuri katika dakika ya 52, kwa shuti la kuzungusha, ambapo Juan Mata
alipachika goli la pili kwa mkwaju wa penati baada ya Anthony
Martial, kuchezewa rafu na Gareth McAuley aliyepewa kadi nyekundu kwa
kosa hilo.
Matokeo mengine ya mechi za Ligi Kuu
ya Uingereza ni, Bournemouth 0 - 1 Newcastle, Leicester 2 - 1
Watford, Norwich 1 - 0 Swansea, Sunderland 0 - 1 Southampton na West
Ham 1 - 1 Everton.




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni