Filamu fupi ya nyota wa soka duniani
Cristiano Ronaldo imezinduliwa Jijini London huku Sir Alex Ferguson
akijiunga na mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United katika
uzinduzi huo uliofanyika jana jioni.
Mchezaji huyo wa Real Madrid mwenye
umri wa miaka 30 alikuwa huko Leicester Square Uingereza kuangalia
kwa mara ya kwanza filamu hiyo fupi iliyoongozwa na James Gay-Rees
na kupatiwa jina la 'Ronaldo'.
Filamu hiyo fupi imetengenezwa kwa
miezi 14, wakati Ronaldo akishinda Kombe Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na
Real Madrid mwaka 2014. Jose Mourinho, Carlo Ancelotti, Radamel
Falcao, Gary Neville pamoja na Louis Saha walihudhuria pia uzinduzi
huo.
Ronaldo akiwa na Sir Alex Ferguson
Ronaldo akiwa na kocha Carlo Ancelotti na wakala
Jorge Mendes
Kocha Jose Mourinho akiingia ukumbini kuangalia filamu hiyo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni